Batuli Afunguka Kuhusu Mambo ya Chumbani na Nguo za Ndani Anazopendelea Kuvaa
STAA wa sinema za Kibongo, Yobnesh
Yusuf 'Batuli' amefungukia mambo yake ya
chumbani na kuanika kuwa anapenda
kuvaa kufuli zenye rangi tofauti.
Akizungumza na Gpl, Batuli ambaye
anaendelea kufanya vizuri Bongo Movies
kila kukicha, alisema kama binadamu
wengine na yeye linapofika suala la viwalo
hivyo vya ndani, anapenda kununua vingi
vyenye rangi tofauti.
"Nanunua nyingi lakini sipendi ziwe za
rangi moja hivyo siwezi kununua dazeni
nzima ila nanunua chachechache sehemu
tofauti ili niweze kupata rangi tofauti,"
alisema Batuli huku akibanwa zaidi na
mwandishi:
Mwandishi: Mpenzi wako anapotoka kazini
na kuja kwako huwa unapenda kumfanyia
nini?
Batuli: Nina utundu wangu kama
mwanamke, ila ni siri yangu.
Mwandishi: Nyakati za usiku unapokuwa
nyumbani muda wa kwenda kulala,
unapenda kumpigia simu nani kama mtu
wa mwisho?
Batuli: Kwanza mpenzi wangu anapokuwa
hayupo, wazazi wangu na watoto wangu
wawili walioko shule.
Mwandishi: Hebu tuambie nini siri ya
urembo wako?
Batuli: Ni kujizuia sana na ulevi, lakini pia
huwa nakuwa makini na mwili wangu,
mpenzi wangu pia anachangia urembo
wangu pamoja na kujipangia ratiba nzuri
ya chakula maana si kila chakula naweza
kula.
Mwandishi: Ulishawahi kutoa mimba?
Batuli: Sijawahi na sitaki ila nina watoto
Post a Comment